Wawakilishi wa cocacola wakimkabidhi Le Mutuz zawadi ya Kopo la kwanza lenye jina lake leo at downtown bongo!! |
Monday, 12 January 2015
COCACOLA YAMKABIDHI LE MUTUZ ZAWADI YA KOPO LA SODA LENYE JINA LAKE LITAKALOANZA KUUZWA MTAANI KARIBUNI
MBUNGE WA VITI MAALUM WA CCM MKOA WA ARUSHA MH. CATHERINE MAGIGE AZINDUA RASMI DUKA LA ZURII HOUSE OF BEAUTY LILILOPO DAR FREE MARKET
Gari la DC wa Mbozi lazua tafrani jimboni kwa Kilango
Same. Katika hali isiyo ya kawaida, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, Dk Michael Kadege limekutwa likipeperusha bendera katika eneo la Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na kuzua tafrani kati ya mkuu huyo na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.
Gari hilo likiwa na Bendera ya Taifa, lilionekana
saa nne asubuhi likiwa limeegeshwa katika eneo la Mamba Myamba katika
Jimbo la Same Mashariki huku Dk Kadege akiwa kwenye mgahawa.
Kitendo cha gari hilo kuonekana likipeperusha
bendera kilimfanya Kilango kulifuata akidhani ni la Mkuu wa Wilaya ya
Same, ndipo akakuta ni la Mbozi.
“Hili gari siyo la Same na kawaida mkuu wa wilaya
nyingine haruhusiwi kupeperusha bendera kwenye eneo ambalo siyo lake,
huyu amekuja kwenye mambo yake ya siasa, anapeperusha bendera ili
wananchi wamwone kuwa yuko juu na hii ni hujuma kwenye jimbo langu,”
alilalamika Kilango.
Alisema Dk Kadege ni miongoni mwa watu wanaotaka
kugombea ubunge Jimbo la Same Mashariki lakini ni vyema akasubiri muda
ukifika ajitokeze hadharani badala ya kujenga mpasuko kwa CCM katika
jimbo hilo.
“Huyu amekuja kwa ajili ya vikao vya ndani, mwaka
2005 tuligombea wote kwenye kura za maoni nikamshinda nikiwa na kura 389
yeye 46 akawa mtu wa nne, mwaka 2010 mimi nilipata kura 7,900 na yeye
alipata 2,200 sasa ameanza, sikatai lakini asubiri muda wake,” alisema
Kilango.
Kwa upande wake, Dk Kadege alisema hakuwa na
taarifa kuwa gari lake linapeperusha bendera kwa kuwa yeye hahusiki
kuweka bendera, akataka dereva wake aeleze sababu za kupeperusha bendera
kwenye eneo lisiloruhusiwa.
Dk Kadege alisema yeye yuko likizo na alikwenda
nyumbani kwao Same kupumzika na hafanyi shughuli zozote za kisiasa
katika jimbo hilo kama inavyodaiwa na Kilango.
Dereva wa mkuu huyo wa wilaya ambaye alikataa
kutaja jina lake, alipohojiwa sababu za kupeperusha bendera katika eneo
lisiloruhusiwa alisema alikuwa akifanya usafi wa gari na alipohojiwa
zaidi alidai siyo msemaji wa mkuu wa wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi alisema
kutokana na sheria, utaratibu na miongozo ya wakuu wa wilaya, kiongozi
huyo wa wilaya haruhusiwi kupeperusha bendera katika eneo ambalo siyo
lake.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa
namba 19 ya Mwaka 1997 na Sheria ya Serikali za Mitaa namba Saba na Nane
ya mwaka 1982, mkuu wa wilaya ni msimamizi wa shughuli za kimaendeleo
na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya yake tu.
Kapufi alisema atawasiliana na Dk Kadege kama
anafahamu utaratibu na miongozo waliyopewa wakati wa kuanza kazi ili
ajue kama alikusudia kufanya hivyo au kama alipitiwa.
Chanzo Gazeti la Mwananchi
Chanzo Gazeti la Mwananchi
Thursday, 27 November 2014
Familia Kasigwa Mzee inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa Eustadius D.Kasigwa
Tuesday, 25 November 2014
TUMWEZESHE DADA HUYU
Katika maisha yetu Mungu anatuinua ili na sisi tuweze kuwainua wengine.Tunakutana na watu wenye shida na tunatumia nafasi tulizonazo kuwapa mwanga.Dada Dina Cares foundation kwa kushirikiana na CSMF na kupewa nguvu na Nyama choma festival tunamleta kwenu dada Hafna ambae ni single mother.Tunamuwezesha kupata vitu ambavyo vitamfanya aweze kumudu kuwa na banda la kuchoma nyama siku ya nyama choma festival tarehe 6 dec.Tunakukaribisha kumuwezesha Mchango wako wa pesa au kama mtu unaweza kuwasiliana nae ukampelekea Nyama (Ng'ombe/Mbuzi/Kuku) Viazi, Ndizi Mzuzu, Mkaa,Mafuta Ya Kupikia n.k
Lengo ni yeye afanye kazi na kupitia kazi hiyo aweze kupata mtaji wa kujiajiri mwenyewe.
Nyama Choma festival wamempa banda bure,mbuzi mmoja,kuku watano na kigunia cha mkaa.Dada dina cares itampa mbuzi mmoja,kuku watano na ndoo ya mafuta.Hivi havitoshi tunakukaribisha umchangie ili afikie malengo yake.
Namba ya mpesa ipo kwenye hiyo posta kama huoni vizuri ni hii hapa 0768 835184.
Na kwa support zaidi pls repost hii iweze kuwafikia wengi.
SASA KUMEKUCHA!!!! IPTL WATINGA MAHAKAMANI KUZUIA BUNGE KUJADILI WIZI WA FEDHA WA ESCROW HAPO JANA
Posted by
edward michael
On
3:32 AM
|
No comments
IMEANDIKWA NA SAED KUBENEA
IPTL WATINGA MAHAKAMANI KUZUIA BUNGE
Kampuni ya PAN Africa Power Sulition (PAP), wamefungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, asubuhi hii, kuomba mahakama itoe amri ya zuio la muda la kuzuia bunge kujadili wizi wa fedha kwenye akaunti ya Escrow.
Kesi hiyo ni Misc Civil Application Na. 50 ya 2014 ambayo ni kesi ya msingi na maombi ya zuio ni Misc Civil Application 51 2014 a- Injunction - ambako pamoja na mengine, mahakama imeobwa kutoa amri ya kulizuia bunge kujadili Escrow akaunti.
Washitakiwa katika kesi hii, ni Spika wa Bunge, Katibu wa Bunge, CAG, TAKUKURU na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini. Kumekucha!
HUU NDIO UKWELI: Mama wa mtoto aliyeteswa na mfanyakazi wa ndani asimulia, mfanyakazi afunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua!
Mfanyakazi
wa ndani ambaye video iliyosambaa mtandaoni inamuonesha akimpiga
kikatili mtoto mdogo, amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua.
Jolly Tumuhirwe, mfanyakazi huyo wa ndani kwenye video hiyo anashikiliwa kwenye mahabusu ya gereza la Luzira, Kampala nchini Uganda na anatarajiwa kupanda kizimbani December 8.
Mtoto huyo kwenye video anaitwa Arnella Kamanzi ambaye pamoja na kuonekana mcheshi, anaendelea kukumbuka mateso aliyoyapata kiasi kwamba hakubali tena kubebwa na mtu asiyemfahamu.
Jolly Tumuhirwe, mfanyakazi huyo wa ndani kwenye video hiyo anashikiliwa kwenye mahabusu ya gereza la Luzira, Kampala nchini Uganda na anatarajiwa kupanda kizimbani December 8.
Mtoto huyo kwenye video anaitwa Arnella Kamanzi ambaye pamoja na kuonekana mcheshi, anaendelea kukumbuka mateso aliyoyapata kiasi kwamba hakubali tena kubebwa na mtu asiyemfahamu.
Mtoto, Arnella Kamanzi
Kwa
siku tatu hizi, mtoto Arnella mwenye miezi 18, amekuwa gumzo kwenye
mitandao ya kijamii Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, kutokana na
video hiyo inayomuoneshwa akipigwa bila huruma na mfanyakazi huyo.
Mama yake, Angella Mbabazi bado anaendelea kuumizwa na walichokishuhudia kwenye video hiyo kiasi ambacho hulia kila anaposimulia. “Mfanyakazi mwingine alimpendekeza kwetu. Alituambia kuwa alikuwa anatokea kijiji cha Rukungiri. Ni baada tu ya tukio hili baya alituambia kuwa alikuwa mfanyakazi huko Nakulabye kabla ya kuja hapa,” aliliambia gazeti la Daily Monitor la Uganda.
Mama yake, Angella Mbabazi bado anaendelea kuumizwa na walichokishuhudia kwenye video hiyo kiasi ambacho hulia kila anaposimulia. “Mfanyakazi mwingine alimpendekeza kwetu. Alituambia kuwa alikuwa anatokea kijiji cha Rukungiri. Ni baada tu ya tukio hili baya alituambia kuwa alikuwa mfanyakazi huko Nakulabye kabla ya kuja hapa,” aliliambia gazeti la Daily Monitor la Uganda.
MUHIMU SANA: FAHAMU JUU YA KUCHANGIA DAMU KWA MAMA MJAMZITO (MASWALI NA MAJIBU) SOMA HAPA
Aina za damu
Aina
ya damu (pia huitwa kikundi cha damu) ni uainishaji wa damu kwa
kuzingatia kuwepo au kutokuwepo kwa dutu za antijeni za kurithiwa kwenye
uso wa chembechembe nyekundu za damu (RBCs). Aina ya damu (Kikundi cha
damu) inaamuliwa kwa sehemu, na antijeni za aina ya damu ya ABO zilizo
kwenye chembechembe nyekundu za damu.
Aina
za damu huathiriwa na huwakilisha michango kutoka kwa wazazi wote
wawili. Jumla ya mifumo 30 ya aina ya damu ya binadamu (ikiwa ni pamoja
na mifumo ya ABO & Rh) sasa inatambuliwa na Shirika la Kimataifa la
Upaji wa Damu (ISBT).
Aina
ya damu kamili ni seti kamili ya dutu 30 kwenye uso wa chembechembe
nyekundu za damu na aina ya damu ya mtu ni mojawapo ya miungano
iwezekanayo ya antijeni za aina ya damu. Katika aina hizo 30 za damu,
zaidi ya antijeni 600 tofauti za aina ya damu zimepatikana, lakini
nyingi ya hizi ni nadra sana au kwa kiasi kikubwa hupatikana katika
makabila fulani.
Mfumo wa ABO ni mfumo muhimu zaidi wa aina ya damu katika
kuongezewa damu kwa binadamu. Kingamwili kinza-A na kingamwili kinza-B zinazohusika kwa kawaida ni kingamwili za Immunoglobulini M, inayofupishwa IgM. Mfumo wa Rh ni mfumo wa pili muhimu zaidi wa aina ya damu katika kuongezewa damu kwa binadamu ukiwa na antijeni 50 kwa sasa.
kuongezewa damu kwa binadamu. Kingamwili kinza-A na kingamwili kinza-B zinazohusika kwa kawaida ni kingamwili za Immunoglobulini M, inayofupishwa IgM. Mfumo wa Rh ni mfumo wa pili muhimu zaidi wa aina ya damu katika kuongezewa damu kwa binadamu ukiwa na antijeni 50 kwa sasa.
Wanawake
wengi wajawazito hubeba kijusi kilicho na aina ya damu tofauti na yao
na mama huweza kutengeneza kingamwili dhidi ya chembechembe nyekundu za
damu za kijusi. Wakati mwingine kingamwili hizi za mama zinaweza kuvuka
kondo na kusababisha hemolosia ya chembechembe nyekundu za damu, ambayo
inaweza kusababisha ugonjwa wa hemolitiki wa mtoto mchanga (HDN),
ugonjwa wa hesabu ya chini ya damu ya kijusi.
Karibu
kila mara, mtu ana aina moja ya damu maisha yake yote, lakini mara
chache sana aina ya damu ya mtu hubadilika kwa sababu ya kuongezeka au
ukandamizaji wa antijeni katika maambukizi, donda ndugu au ugonjwa kinga
mwili nafsi.
Aina/Makundi ya damu na Upatanifu wa Chembechembe nyekundu za Damu
- Watu wenye damu ya aina ya AB wana antijeni zote mbili za A na B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu na majimaji yao ya damu hayana kingamwili zozote dhidi ya antijeni A au B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya AB anaweza kupokea damu aina yoyote (aina ya AB inapendekezwa) lakini anaweza kutoa damu kwa mwingine mwenye aina ya AB pekee.
- Watu wenye damu ya aina ya A wana antijeni ya A kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu na majimaji yao ya damu yana kingamwili za IgM dhidi ya antijeni ya B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya ya A anaweza kupokea damu kutoka kwa watu wenye aina ya A au 0 pekee (aina ya A inapendekezwa) na anaweza kutoa damu kwa watu wengine wenye aina ya A au AB.
- Watu wenye damu ya aina ya B wana antijeni ya B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu na majimaji yao ya damu yana kingamwili za IgM dhidi ya antijeni ya A. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya B anaweza kupokea damu kutoka kwa watu wenye aina ya B au O (aina ya B inapendekezwa) na wanaweza kutoa damu kwa watu wenye aina ya B au AB.
- Watu wenye damu ya aina ya O (au kikundi cha damu cha sifuri katika nchi kadhaa) hawana antijeni A au B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu lakini majimaji yao ya damu yana kingamwili kinza-A na kingamwili kinza-B za IgM dhidi ya antijeni za aina ya damu za A na B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya 0 anaweza tu kupokea damu kutoka kwa mtu mwenye aina ya 0, lakini anaweza kutoa damu kwa watu wa aina yoyote ya ABO (yaani kundi A, B, AB & O).
Masuala ya kuzingatia kabla ya kuchangia damu kwa mama mjamzito
Kabla ya Kuchangia damu
- Zingatia ulaji wa vyakula vyenye madini chuma kama nyama nyekundu (mfano nyama ya ng'ombe), samaki, maharage n.k
- Pata chakula bora chenye afya yaani mlo kamili. Epuka vyakula vyenye mafuta hasa vilivyokaangwa.
- Kunywa maji mengi angalau glasi 6 hadi 8.
- Pata usingizi mzuri wa usiku.
- Kumbuka kuwa na kitambulisho chako chochote.
Wakati wakuchangia damu
- Vaa nguo inayoweza kukunjwa hadi juu ya kiwiko.
- Muonyeshe mtoa damu mkono unaotaka utolewe damu, ikiwezekana muonyeshe na mshipa uliofanikisha kutolewa damu wakati uliopita kama umewahi kuchangia damu.
- Kuwa mtulivu wakati wa kutolewa damu ikiwezekana ongea na mchangiaji damu aliyekaribu yako au sikiliza muziki wa taratibu.
- Punde umalizapo kuchangia damu, tumia muda wako kufurahia vyakula na vinywaji laini vilivyoletwa na wahamasishaji wa kuchangia damu.
Baada ya kuchangia damu
- Kunywa maji mengi zaidi na jiepushe na pombe ndani ya masaa 24 yajayo.
- Ondoa bandeji/pamba iliyowekwa pale ulipotobolewa kuzuia damu isitoke baada ya saa 1 baada ya kuchangia damu.
- Sehemu iliyochomwa sindano kama bado inatoa damu, izibe kwa nguvu na pamba kavu kisha nyoosha mkono juu kwa dakika 5 hadi 10.
- Ili kuepuka maambukizi ya ngozi na muwasho osha kwa maji na sabuni sehemu ya mwili iliyotumika kutoa damu.
- Usifanye kazi ngumu yoyote kama kubeba vitu vizito ndani ya siku yote ambayo umetoa damu.
- Kama unasikia kizunguzungu na kuishiwa nguvu & pumzi baada ya kuchangia damu unapaswa kukaa chini au kulala hadi utakapojisikia vizuri.
- Kula vyakula vyenye protini kwa wingi baada ya kuchangia damu mfano nyama ya ng'ombe, kuku, kunde n.k
Mawali na majibu juu ya Uchangiaji damu
Inachukua muda gani kuchangia damu?
Hatua
zote mpaka damu kuwa imetolewa inachukua kama saa moja na dakika 15.
Muda mahususi kwa kutoa damu chupa moja ya damu ni dakika 8 hadi 10,
ingawa muda hutofautiana kwa sababu tofauti kama hali ya afya ya
mchangia damu na mahudhurio ya sehemu za kuchangia damu.
Wakati gani mjamzito hupungukiwa damu?
Upungufu
wa damu wakati wa ujauzito unaweza kutokea katika mabidiliko ya kawaida
ya ujauzito ambapo chembechembe nyekundu huongezeka kwa kiwango kidogo
kuliko maji(Physiological hemodilution), hata hivyo mabadiliko haya
yanaweza kurekebishwa kwa kutumia madini chuma na folic acid bila
kuhitaji kuongezewa damu. Matatizo yanayoweza kusababisha upungufu
mkubwa mpaka kuhitaji kuongezewa ni pamoja na lishe duni(isiyo na madini
chuma na vitamin stahiki), maambukizi ya minyoo, malaria, kupasuka kwa
mimba iliyotungwa nje ya mfuko wa uzazi (Ruptered Ectopic Pregnancy),
kutoka/kutoa mimba, kutokwa damu ukeni kabla, wakati wa kujifungua na
baada ya kujifungua.
Mama mjamzito huhitaji kuchangiwa damu wakati upi?
Mama
mjamzito huhitaji kuchangiwa damu wakati wowote kabla hajapata matatizo
yatakayopelekea kupungukiwa damu. Damu inaweza kuhifadhiwa na kusubiri
hali ya dharula ikitokea.
Nini madhara ya mjamzito kupungukiwa damu?
Upungufu
wa damu wa muda mrefu unaweza athiri maisha ya mama na mtoto
aliyetumboni.Mama anaweza kujikuta moyo ukashindwa kufanya kazi vizuri
na kupoteza maisha. Mtoto hataweza kukua vizuri na anaweza fia tumboni
au akazaliwa akiwa na uzito mdogo sana.Endapo mjamzito atatokwa na damu
nyingi sana ukeni kabla ya kujifungua au baada ya kujifungua anaweza
kuishiwa nguvu kabisa, kuzimia au hata kupoteza maisha.
Nini hufanyika baada ya kuishiwa damu?
Mgonjwa
hukaguliwa haraka na kujua chanzo cha tatizo lake na kuzuia utokaji wa
damu zaidi, huku wakizuia asizimie/kupoteza fahamu kwa kumpatia huduma
stahiki ikiwa ni pamoja kurejesha kiwango cha maji yaliyopungua mwilini
haraka sana kwa maji ya drip, wakati jitihada za kutafuta kumwongeza
damu zinaendelea.
Wapi watakiwa kwenda kuchangia damu?
Nchini Tanzania, sehemu za kuchangia damu zimegawanyika kikanda kama ifuatavyo :-
(a) Kanda ya Mashariki; inayohudumia mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Dodoma & Pwani. Ofisi kuu za kanda zikiwa Mchikichini, Ilala, Dar es salaam. Simu ni 0715339282.
(b)
Kanda ya Ziwa; inayohudumia mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera &
Shinyanga. Ofisi kuu za kanda zikiwa Mwanza karibu na Hospitali ya
Bugando. Simu ni 0768479381.
(c)
Kanda ya Magharibi; inayohudumia mikoa ya Tabora, Kigoma & Singida.
Ofisi kuu za kanda zikiwa Tabora karibu na Hospitali ya Kitete. Simu
ni 0785733606.
(d)
Kanda ya Kusini; inayohudumia mikoa ya Lindi & Mtwara. Ofisi kuu za
kanda zikiwa Mtwara karibu na Hospitali ya Ligula. Simu ni0786852051.
(e)
Kanda ya Kaskazini; inayohudumia mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha
& Manyara. Ofisi kuu za kanda zikiwa Moshi, Kilimanjaro karibu na
Hospitali ya KCMC. Simu ni 0716231406.
(f)
Kanda ya nyanda za juu Kusini; inayohudumia mikoa ya Mbeya, Iringa
& Songea. Ofisi kuu za kanda zikiwa Mbeya karibu na Hospitali ya
Meta. Simu ni 0767502430.
Mawali na majibu zaidi juu ya Uchangiaji damu
Swali : Nitalipwa nikichangia damu?
Jibu : Hapana. Hakuna malipo baada ya kuchangia damu. Wachangiaji hutoa damu kwa kujitolea kwa hiari yao.
Swali : Je, ni salama kwa mjamzito kuchangiwa damu?
Jibu : Ni salama kwa kuwa vigezo vyote vya usalama huchukuliwa kwa uzito.
Swali : Je, ni kweli kuwa kila kundi la mchangia damu lazima liwe sawa na mjamzito anayechangiwa?
Jibu
: Kwa kawaida damu ya mchangiaji hukusanywa bila kujali ni kundi gani,
endapo mjamzito atahitaji kutiwa damu ndipo kundi la damu ya mchangiaji
litatafutwa ili kuendana na kundi la mjamzito.
Swali : Kuna faida gani kuchangia damu?
Jibu
: Kuokoa maisha, kufahamu kundi lako la damu, kufahamu hali yako ya
maambukizi ya magonjwa kama UKIMWI, Kaswende na Mchochota wa aina B
& C, pia ni uzalendo.
Swali : Kuna hasara gani anayopata mchangia damu tokana na kuchangia damu?
Jibu : Hakuna hasara anayopata mchangiaji damu kwa kuwa damu atakayochangia itatumika kuokoa maisha ya wenye uhitaji wa damu.
Swali : Je, damu huuzwa kwa wanaohitaji?
Jibu : Hapana, damu haiuzwi na hutolewa bure kwa anaehitaji
Swali : Ni kina nani watakaopata damu niliyochangia?
Jibu
: Watu wenye upungufu wa damu hasa watoto, watu waliofanyiwa upasuaji
mkubwa, wagonjwa wenye saratani, majeruhi wa ajari na kina mama
wajawazito wenye matatizo ya uzazi kama kutokwa damu nyingi baada ya
kujifungua.
Swali : Ni magonjwa gani yanaweza kusambazwa kwa njia ya damu?
Jibu : Magonjwa mengi husambazwa kwa njia ya damu kama UKIMWI, Kaswende & Mchochota wa aina B & C na bacteria.
Swali : Je, unaweza kupata maambukizi ya UKIMWI ukichangia damu?
Jibu
: Hapana kabisa. Sindano na vifaa vingine vyenye ncha kali
vinavyotumika ni safi & salama. Watumishi wa ukusanyaji damu
wanafuata viwango vya usalama na kuzuia maambukizi kama
walivyofundishwa.
Swali : Je, ni salama kuchangia damu?
Jibu
: Ndiyo, ni salama kuchangia damu kwa kuwa kabla ya kuchangia damu mtu
hukaguliwa na kuulizwa maswali kuona kama amekidhi vigezo vya kuchangia
damu ikiwa ni pamoja na kuangaliwa wingi wa damu na kupimwa shinikizo la
damu.
Swali : Ninaweza kuchangia damu ikiwa sijala?
Jibu
: Ukichangia damu hujala unaongeza hatari ya kupata matatizo baada ya
kuhangia damu, hivyo inashauriwa kula chakula chepesi ndani ya masaa 4
baada ya kuchangia damu.
Swali : Ni damu kiasi gani huchukuliwa kwa wakati mmoja?
Jibu : Ni kiasi cha Mililita 480 za damu ndio kiwango kinachokubaliwa kisheria.
Swali : Ninaweza kutoa damu kila baada ya muda gani?
Jibu
: Unaruhusiwa kuchangia damu kila baada ya siku 52 ili kuhakikisha
mwili umepata muda wa kutosha kurudisha chembechembe za damu zilizopotea
baada ya kuchangia damu wakati uliopita.
Swali : Ninahitaji kula mlo maalumu baada ya kuchangia damu?
Jibu : Hapana, endelea na mlo wako wa kila siku pia unaweza kuhakikisha ni mlo kamili tu.
Swali : Itachukua muda gani kwa mwili kurudisha kiwango cha damu nilichokitoa?
Jibu : Sehemu ya maji (Plasma) ya damu huweza kuridi ndani ya masaa 24 wakati chembechembe za damu hurudi baada ya wiki mbili.
Swali : Je, damu yangu itapimwa magonjwa kama UKIMWI kabla sijatoa?
Jibu : Hapana, hutolazimika kupima UKIMWI kama hauko tayari kufanya hivyo.
Swali : Damu salama ni nini?
Jibu : Damu salama ni ile imepimwa na kuonekana haina UKIMWI, Kaswende, Mchochota wa aina B & C wala vimelea vya bacteria.
Swali : Nitapata wapi majibu yangu ya vipimo nilivyofanya wakati wa uchangiaji damu?
Jibu : Utapata majibu katika ofisi za damu salama zilizo karibu nawe au pale ulipochangia damu.
Swali : Nani anaruhusiwa kumchangia damu mama mjamzito?
Jibu
: Mtu yoyote mwanamke au mwanaume anaweza kumchangia damu mama mjamzito
ikiwa ana afya njema na anajisikia vizuri, umri kati ya miaka 18 hadi
65, uzito usiopungua kilo 50, wingi wa damu zaidi ya gramu 12 kwa
desilita, kutokuwa na shinikizo la juu la damu na kwa mwanamke asiwe
mjamzito au anayenyonyesha.
Monday, 24 November 2014
KAMPUNI YA MABATI YA ALAF YATOA MSAADA WA MABATI KWA AJILI YA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA MBEYA.
Meneja
wa Kampuni ya ALAF Tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege akitoa taarifa kwa
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kabla ya kumkabidhi msaada wa mabati 384 kwa
ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King, akitoa shukrani kwa kampuni ya ALAF kwa kujitolea mabati kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari za Wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King na Meneja wa ALAF tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege wakikabidhiana mabati 284 kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za Kata.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King akiwaonesha waandishi wa
habari(hawapo pichani) msaada wa mabati aliyokabidhiwa na Kampuni ya ALAF .
Meneja wa ALAF tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya bidhaa zingine zinazozalishwa katika kiwanda cha Mbeya.
Fundi
umeme na mtaalamu wa Mashine wa Kiwanda cha kuzalisha mabati, Himid
Mwenzegule akiendelea kuendesha mitambo ya mashine ya kuzalisha mabati
kiwandani hapo.
Mashine ya kuzalisha mabati ya migongo ya kawaida aina ya Corrugator ikiendelea na kazi.
Mashine ya kuzalisha mabati ya migongo mikubwa aina ya IT.
Mashine ya kuzalisha vigae aina ya Versa Tile
Mabati aina ya Simba Dumu yaliyozalishwa kiwandani hapo.
Baadhi ya mabati yaliyozalishwa kiwandani hapo yakiingizwa kwenye Roli tayari kuelekea sokoni kwa wateja.
KAMPUNI ya mabati ya ALAF imetoa msaada
wa mabati 384 kwa ajili ya ujenzi wa maabara za shule za Sekondari za
Wilaya ya Mbeya zenye thamani ya shilingi Milioni 7.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk.
Norman Sigallah King,Meneja wa Tawi la Mbeya Greyson Mwakasege, alisema
walipokea maombi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kwa ajili ya
kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule za Kata.
Alisema
walikubaliana na ombi hilo na kuona ni vema kusaidia Bandle 32 sawa na
mabati 384 yenye thamani ya Shilingi Milioni 7 baada ya mabati hayo
kuanza kuzalishwa katika Kiwanda cha Mbeya ambacho pia kinahudumia Mikoa
ya Ruvuma, Katavi, Rukwa,Njombe, Iringa na Mbeya.
Alisema
ni matarajio yao ya kuendelea kusaidia maeneo mengine kama mchango wa
Kampuni kwa jamii inayowazunguka pamoja na kuthamini wateja wake ambao
hupata huduma kutoka katika kiwanda cha Mbeya.
Mwakasege
aliongeza kuwa katika Kiwanda cha Mbeya kina mashine tatu ambazo ni
Mashine aina ya IT inayotengeneza mabati ya migongo mikubwa, Mashine
aina ya Corrugator inayozalisha mabati yenye migongo ya kawaida midogo
pamoja na mashine aina ya Versa Tile inayozalisha vigae aina ya Versa.
Alizitaja
bidhaa zingine zinazopatikana kuwa ni pamoja na Bati za Afrika kusini
na vigae vyenye rangi za Bluu, Kijani na Nyekundu,Nondo kutoka Uturuki,
Black Pipe, Z parlin na Hollow section.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King, mbali na kutoa shukrani kwa Kampuni ya ALAF kwa
msaada wa mabati pia alitoa wito kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Mbeya
kujenga utamaduni wa kuchangia shughuli za maendeleo ya Wilaya.
Alisema
mabati hayo yatasaidia katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana
ya Galijembe ambayo imeteuliwa na Wilaya kuwa Shule ya Bweni ya
wasichana kutokana na ujenzi wa maabara kukamilika kwa asilimia kubwa.
Alisema
lengo la kuiteua shule ya Galijembe kuwa shule ya Wasichana ya bweni ya
Wilaya ni kuwaondolea adha watoto wa kike ambao asilimia kubwa wanaumri
mdogo kwenda uaraiani kupanga vyumba baada ya kufaulu kujiunga na
sekondari.
Alisema
wasichana wanapata madhara makubwa wakiwa wamepanga kwenye nyumba
uaraiani yakiwemo Mimba za utotoni na magonjwa ikiwa ni pamoja na
kupunguza hali ya ufaulu darasani kutokana na mazingira hivyo Wilaya ya
Mbeya imejipanga kuhakikisha hilo linaondoka.
Subscribe to:
Posts (Atom)