Meneja
wa Kampuni ya ALAF Tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege akitoa taarifa kwa
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kabla ya kumkabidhi msaada wa mabati 384 kwa
ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King, akitoa shukrani kwa kampuni ya ALAF kwa kujitolea mabati kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari za Wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King na Meneja wa ALAF tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege wakikabidhiana mabati 284 kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za Kata.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King akiwaonesha waandishi wa
habari(hawapo pichani) msaada wa mabati aliyokabidhiwa na Kampuni ya ALAF .
Meneja wa ALAF tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya bidhaa zingine zinazozalishwa katika kiwanda cha Mbeya.
Fundi
umeme na mtaalamu wa Mashine wa Kiwanda cha kuzalisha mabati, Himid
Mwenzegule akiendelea kuendesha mitambo ya mashine ya kuzalisha mabati
kiwandani hapo.
Mashine ya kuzalisha mabati ya migongo ya kawaida aina ya Corrugator ikiendelea na kazi.
Mashine ya kuzalisha mabati ya migongo mikubwa aina ya IT.
Mashine ya kuzalisha vigae aina ya Versa Tile
Mabati aina ya Simba Dumu yaliyozalishwa kiwandani hapo.
Baadhi ya mabati yaliyozalishwa kiwandani hapo yakiingizwa kwenye Roli tayari kuelekea sokoni kwa wateja.
KAMPUNI ya mabati ya ALAF imetoa msaada
wa mabati 384 kwa ajili ya ujenzi wa maabara za shule za Sekondari za
Wilaya ya Mbeya zenye thamani ya shilingi Milioni 7.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk.
Norman Sigallah King,Meneja wa Tawi la Mbeya Greyson Mwakasege, alisema
walipokea maombi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kwa ajili ya
kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule za Kata.
Alisema
walikubaliana na ombi hilo na kuona ni vema kusaidia Bandle 32 sawa na
mabati 384 yenye thamani ya Shilingi Milioni 7 baada ya mabati hayo
kuanza kuzalishwa katika Kiwanda cha Mbeya ambacho pia kinahudumia Mikoa
ya Ruvuma, Katavi, Rukwa,Njombe, Iringa na Mbeya.
Alisema
ni matarajio yao ya kuendelea kusaidia maeneo mengine kama mchango wa
Kampuni kwa jamii inayowazunguka pamoja na kuthamini wateja wake ambao
hupata huduma kutoka katika kiwanda cha Mbeya.
Mwakasege
aliongeza kuwa katika Kiwanda cha Mbeya kina mashine tatu ambazo ni
Mashine aina ya IT inayotengeneza mabati ya migongo mikubwa, Mashine
aina ya Corrugator inayozalisha mabati yenye migongo ya kawaida midogo
pamoja na mashine aina ya Versa Tile inayozalisha vigae aina ya Versa.
Alizitaja
bidhaa zingine zinazopatikana kuwa ni pamoja na Bati za Afrika kusini
na vigae vyenye rangi za Bluu, Kijani na Nyekundu,Nondo kutoka Uturuki,
Black Pipe, Z parlin na Hollow section.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King, mbali na kutoa shukrani kwa Kampuni ya ALAF kwa
msaada wa mabati pia alitoa wito kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Mbeya
kujenga utamaduni wa kuchangia shughuli za maendeleo ya Wilaya.
Alisema
mabati hayo yatasaidia katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana
ya Galijembe ambayo imeteuliwa na Wilaya kuwa Shule ya Bweni ya
wasichana kutokana na ujenzi wa maabara kukamilika kwa asilimia kubwa.
Alisema
lengo la kuiteua shule ya Galijembe kuwa shule ya Wasichana ya bweni ya
Wilaya ni kuwaondolea adha watoto wa kike ambao asilimia kubwa wanaumri
mdogo kwenda uaraiani kupanga vyumba baada ya kufaulu kujiunga na
sekondari.
Alisema
wasichana wanapata madhara makubwa wakiwa wamepanga kwenye nyumba
uaraiani yakiwemo Mimba za utotoni na magonjwa ikiwa ni pamoja na
kupunguza hali ya ufaulu darasani kutokana na mazingira hivyo Wilaya ya
Mbeya imejipanga kuhakikisha hilo linaondoka.
No comments:
Post a Comment