Pages

Monday, 12 January 2015

MBUNGE WA VITI MAALUM WA CCM MKOA WA ARUSHA MH. CATHERINE MAGIGE AZINDUA RASMI DUKA LA ZURII HOUSE OF BEAUTY LILILOPO DAR FREE MARKET

Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe katika ufunguzi wa ZuRii House of Beauty duka jipya na la kisasa la vipodozi lililofunguliwa rasmi leo Jumatatu 12 Jan 2015 Kushoto ni  ni Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George












MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige  leo amezindua rasmi  duka  jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi  Jijini Dar es Salaam.

Akizindua duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza  nyumbani hali ambayo imeweza kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.
“Kabla ya yote nachukua fursa hii kumpongeza  Jestina  kwani ameonesha  mfano  wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa  kwa wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.

Aidha alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine  pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina  alisema kwamba yeye ameona  fursa za  kuwekeza nyumbani  hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.

“Natoa wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja likizo nyumbani nakuinjoi tu  fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru  Mungu kwa kutimiza ndoto hii”.   

Wasiliana nao kwa kuwafollow kupitia acc yao personal ya  

Instagram
@officialjestinageorgeblog au @zuriihouseofbeauty
Contact details +255 752 019 597 au +255 65 918 9769 Whatsapp ni +447557304940 (Business Enquires Only Please).....

No comments: