Pages

Tuesday, 25 November 2014

HUU NDIO UKWELI: Mama wa mtoto aliyeteswa na mfanyakazi wa ndani asimulia, mfanyakazi afunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua!

Mfanyakazi wa ndani ambaye video iliyosambaa mtandaoni inamuonesha akimpiga kikatili mtoto mdogo, amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua. 

Jolly Tumuhirwe, mfanyakazi huyo wa ndani kwenye video hiyo anashikiliwa kwenye mahabusu ya gereza la Luzira, Kampala nchini Uganda na anatarajiwa kupanda kizimbani December 8. 

Mtoto huyo kwenye video anaitwa Arnella Kamanzi ambaye pamoja na kuonekana mcheshi, anaendelea kukumbuka mateso aliyoyapata kiasi kwamba hakubali tena kubebwa na mtu asiyemfahamu.
  Mtoto, Arnella Kamanzi
 
Kwa siku tatu hizi, mtoto Arnella mwenye miezi 18, amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, kutokana na video hiyo inayomuoneshwa akipigwa bila huruma na mfanyakazi huyo. 

Mama yake, Angella Mbabazi bado anaendelea kuumizwa na walichokishuhudia kwenye video hiyo kiasi ambacho hulia kila anaposimulia. “Mfanyakazi mwingine alimpendekeza kwetu. Alituambia kuwa alikuwa anatokea kijiji cha Rukungiri. Ni baada tu ya tukio hili baya alituambia kuwa alikuwa mfanyakazi huko Nakulabye kabla ya kuja hapa,” aliliambia gazeti la Daily Monitor la Uganda.
 
Mama huyo wa watoto wawili alisema kila alipokuwa akijaribu kujua historia yake, Tumuhirwe alikuwa akihama kochi na kuloa jasho na kutoa jibu la neno moja. Ms Mbabazi hakuweza kutambua alama za nyakati zilizoashiria hatari mapema na kujipa moyo kuwa siku moja msichana huyo angemweleza mambo yake.

No comments: