Katika maisha yetu Mungu anatuinua ili na sisi tuweze kuwainua wengine.Tunakutana na watu wenye shida na tunatumia nafasi tulizonazo kuwapa mwanga.Dada Dina Cares foundation kwa kushirikiana na CSMF na kupewa nguvu na Nyama choma festival tunamleta kwenu dada Hafna ambae ni single mother.Tunamuwezesha kupata vitu ambavyo vitamfanya aweze kumudu kuwa na banda la kuchoma nyama siku ya nyama choma festival tarehe 6 dec.Tunakukaribisha kumuwezesha Mchango wako wa pesa au kama mtu unaweza kuwasiliana nae ukampelekea Nyama (Ng'ombe/Mbuzi/Kuku) Viazi, Ndizi Mzuzu, Mkaa,Mafuta Ya Kupikia n.k
Lengo ni yeye afanye kazi na kupitia kazi hiyo aweze kupata mtaji wa kujiajiri mwenyewe.
Nyama Choma festival wamempa banda bure,mbuzi mmoja,kuku watano na kigunia cha mkaa.Dada dina cares itampa mbuzi mmoja,kuku watano na ndoo ya mafuta.Hivi havitoshi tunakukaribisha umchangie ili afikie malengo yake.
Namba ya mpesa ipo kwenye hiyo posta kama huoni vizuri ni hii hapa 0768 835184.
Na kwa support zaidi pls repost hii iweze kuwafikia wengi.
No comments:
Post a Comment